WATU saba wamepoteza maisha katika mapigano ya Wazalendo na Waasi wa M23 RDF katika eneo la Rutchuru, Kivu Kaskazini mwa DRC Congo huku watu zaidi ya 18 wakijeruhiwa.
Ripoti kutoka Shirika la Raia inaeleza kuwa watu hao wamepoteza maisha kutokana na milipuko ya mabomu iliyopiga nyumba zao ikidaiwa kuwa shambulio la waasi wa M23.
Ripoti hiyo inadai kuwa majeruhi wamelazwa katika hospitali ya Bambou wanakoendelea kupatiwa matibabu.
Kwa sasa eneo hilo lipo chini ya udhibiti wa M23 RDF huku hali ikielezwa kuwa ni mbaya na kuna wito kwa serikali ya Kongo kuchukua hatua za haraka kuhakikisha usalama wa raia.
Jean-Claude Bambanze, kiongozi wa shirika la raia wilayani Rutshuru, ameeleza kwamba idadi ya waliofariki ni kubwa, na wengi wamejeruhiwa.
Hofu imetanda kwenye eneo hilo la Rutchuru, Kivu Kaskazini ambako mapambano bado yanaendelea kati ya Wazalendo na Waasi wa M23.
Comments are closed.