Mapigano yaibuka tena eneo la Tigray, Ethiopia

MAPIGANO kati ya wanajeshi kutoka eneo la kaskazini mwa Ethiopia lenye waasi la Tigray na vikosi vya serikali kuu yamezuka karibu na mji wa Kobo ikiwa ni miezi kadhaa tangu wasitishe mapigano, wakaazi wa pande zote mbili walisema Jumatano.

Mapigano hayo ni pigo kubwa kwa matumaini ya mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed na chama cha Tigray People’s Liberation Front (TPLF), chama kinachodhibiti Tigray.

“Saa tano asubuhi leo (TPLF) wameshambulia upande wa Mashariki; kutoka mwelekeo wa Bisober, Zobel na Tekulshe. Kwa kutekeleza hatua kama hiyo, imevunja usitishaji wa mapigano,” huduma ya mawasiliano ya serikali ilisema katika taarifa.

Kamandi ya kijeshi ya vikosi vya Tigraya ilishutumu serikali kwa kukiuka usitishaji huo wa mapigano, ikisema katika taarifa yake inaamini shambulio la kusini lilikuwa ni upotoshaji na vikosi vyao vilitarajia shambulio kubwa kutoka magharibi.

Habari Zifananazo

Back to top button