Mapinduzi 1964 yalivyomng’oa Sultan Jamshid

Mzee Karume

WAZANZIBAR katu hawawezi kuisahau Januari 12, 1964 wala kuipuuza kwani ni siku iliyohitimisha utawala wa kibaguzi wa kisultani kwa kumng’oa, Sultani Jamshid bin Abdullah Al Said.

Ndio maana Januari 12, 2025 Watanzania, yaani Tanganyika (Tanzania Bara) na Zanzibar wanaungana kuadhimisha kumbukumbu ya Miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyoung’oa utawala wa kisultani na ku weka utawala mikononi mwa Wazanzibar wenyewe.

Hii ni siku iliyolinda na kuinua hadhi ya Mzan zibar kupitia Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na kuwafanya Watanzania hawa (Wazanzibar) kuwa huru na wanaostahili na kupata haki sawa, tofauti na ubaguzi na dhuluma waliyofanyiwa tangu utawala wa Kisultani ulipoanza katika visiwa hivyo.

Advertisement

Utawala huo ulikuwa chi ni ya Waarabu walioitawala Zanzibar kabla ya Uingereza kushika hatamu kuion goza Zanzibar mwaka 1890. Uingereza ilishika hatamu hizo hadi Zanzibar ilipopata uhuru Desemba 10, 1963. Hata hivyo licha ya uhuru huo, Zanzibar iliendelea kuwa chini ya utawala wa kisultani kwa kuwa huo uli kuwa ‘uhuru kivuli’ wengine wanasema, ‘uhuru bandia.’

Utawala wa kisultani Zanzibar ulianzishwa na Sultani Seyyid Said mwaka 1840, ukibagua Wazanzibar na kupendelea Waarabu.

Kiu ya Wazanzibar kujitawala, kuheshimika na kujiletea maendeleo dhidi ya ubaguzi haikuishia katika uhuru huo bandia, ndio maana Wazanzibar waliende lea na juhudi zao za kujikom boa hata kufanikiwa kupata ‘uhuru kamili’ mwezi mmoja baada ya kupata uhuru wake, kupitia ya mapinduzi yaliyomwondoa, Sultan Jamshid bin Abdullah Al Said. Mwaka 2024 ‘umekufa’ na Jamshid Jamshid bin Abdullah, sultani wa mwisho kuitawala Zanzibar na aliyeondolewa katika mamlaka kwa Mapinduzi ya Zanzibar, Januari 1964 ‘ameondoka’ amekwenda; amekufa huku akiukumbuka ujasiri, umoja na mshikamano wa Wazanzibar. Jamshid amefariki dunia Desemba 30, 2024 akiwa na umri wa miaka 95.

Baada ya kupinduliwa Zanzibar Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya kihistoria, Sultani Jamshid aliyezaliwa Septemba 16, 1929, Zanzibar na kusoma Alexandria na Beirut, alitawala Zanzibar kuanzia Julai Mosi, 1963 hadi Januari 12, 1964 ukiwa ni muda wa miezi sita tu katika utawala visiwani humo.

Sultan Jamshid

“Hakutawala muda mrefu kwani Wazanzibar hawakuridhika kuwa chini ya utawala wa kisultani ambao ulikuwa wa kibaguzi.

Ubaguzi huo ulienda mbali hadi kufikia hatua ya kusababisha huduma za kijamii kama shule, hospitali na nyingine zo kutolewa kwa misingi ya ubaguzi wa rangi na utajiri,” chanzo kimoja kinasema.

Kinaongeza: “Wazanzibari hawakukata tamaa, bali waliendelea kudai uhuru wao kutoka kwa Sultani wa Zanzibar kwa mapigano makali yakiongozwa na wapiganaji 600 chini ya John Okello.

” Vyanzo vinasema katika harakati hizo za ukombozi wa Wazanzibar kupitia Map induzi ya Zanzibar, Waarabu walizidiwa na maelfu waka toroka visiwa hivyo kuokoa maisha yao. Januari 12, 1964 ukawa mwisho wa utawala wa kisultani katika Visiwa vya Zanzibar.

Mzanzibar akawa huru, akajitawala na kuanza kujiletea maendeleo. Chanzo kinatamka bayana: ‘Utawala wa kisultani haukuwa utawala mwema kwa Wazanzibari kwani uliambatana na biashara ya utumwa na ubaguzi dhidi ya Wazanzibari’.

Inaelezwa kuwa, baada ya kupinduliwa kwa serikali ya kisultani, Jamshid alikimbilia uhamishoni Uingereza kwani nchini Oman, hakupewa hifadhi.

“Kutokana na kushindwa kutawala Zanzibar kama walivyotawala masultani wengine waliopita, Sultan Jamshid hakuruhusiwa kurudi kwao Oman licha ya kutuma maombi mara kadhaa hadi alipofikisha umri wa miaka 50,” chanzo kinasema.

Chapisho hilo linaeleza kuwa, Jamshid alikataliwa maombi yake ya kutaka kuishi nchini Oman ingawa watu wa familia yake waliruhusiwa kuishi nchini humo tangu miaka ya 1980. Aliruhusiwa mwaka 2020 na serikali ya Oman kurejea katika nchi hiyo ya asili ya familia yake kwa sababu ya umri wake.

Kwa kipindi chote alichoishi Uingereza inaripotiwa kuwa, Jamshid aliishi kwa ukimya na hata baadhi ya jirani zake hawakujua yeye ni nani.

Mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964 yaliyoongozwa na Abeid Amani Karume, yalimfanya Jamshid kuwa Sultani wa mwisho kutawala Zanzibar.

Kabla yake, walitawala masultani wengine 12. Sultani wa kwanza alikuwa, Seyyid Said. Jumatano iliyopita makala moja katika HabariLEo iliyokuwa na kichwa cha Habari: ‘Mapinduzi ya Z’bar Yameondoa Unyonge’ iki ema, “Hayo ndiyo Mapin duzi ya Zanzibar; mapinduzi yenye mchango mkubwa katika kupatikana Uhuru wa Tanzania Bara (Tanganyika) huku pia Uhuru wa Tanzania Bara ukiwa na mchango mkubwa katika Mapinduzi ya Zanzibar.”

Inaongeza: “Zanzibar ya sasa baada ya Mapinduzi ni Zanzibar inayoheshimu uhuru, hadhi, haki na maende leo ya watu kisiasa, kielimu, kijamii na hata katika nyanja za utamaduni…”

Inahimiza Watanza nia kuyaenzi Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kwa kuyaishi, kuyaheshimu, kukuza uchumi wa nchi na kukuza uzalendo ili vizazi vijavyo vitakaposherehekea Mapinduzi ya Zanzibar, vikute Zanzibar iliyo bora zaidi. Kwamba, wayaenzi Map induzi ya Zanzibar kwa ku kataa na kukomesha kabisa ubaguzi katika huduma za kijamii kama elimu, afya na nyinginezo.