Mapuri:Lindeni rasilimali za uchaguzi

DAR ES SALAAM : BALOZI wa Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) , Balozi Omar Mapuri, amewataka wasimamizi na waratibu wa uchaguzi nchini kuhakikisha wanasimamia ipasavyo rasilimali, vifaa na fedha za Uchaguzi Mkuu ili zitumike kwa manufaa ya taifa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati akifunga mafunzo ya siku tatu yaliyoshirikisha waratibu wa uchaguzi wa mikoa na wasimamizi wa uchaguzi, wasaidizi wa uchaguzi wa jimbo, maafisa uchaguzi na maafisa ununuzi kutoka mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, Balozi Mapuri amesema vifaa vya uchaguzi vinapaswa kulindwa na matatizo yoyote kuripotiwa mapema.
Hatahivyo ameendelea kusisitiza umuhimu wa kusimamia mafunzo waliyopewa kwa kuzingatia sheria na kanuni, kujiandaa mapema na kuhakiki taarifa kabla ya kukutana na vyombo vya habari wakati wa uchaguzi.SOMA: KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2025: Kataa siasa za uchochezi, hoja za chuki
Wakatihuohuo Mwenyekiti wa mafunzo hayo, Selemani Kateti, amesema washiriki wamejifunza mada 11 ikiwemo majukumu na maadili ya wagombea, mapokezi ya vifaa vya uchaguzi, uchambuzi wa fomu za wagombea na sheria za kampeni.



