Marekani , Iran kujadili mpango wa nyuklia

MAREKANI : RAIS wa Marekani, Donald Trump, ametangaza kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na Serikali ya Iran kuhusu mpango wa nyuklia.

Tangazo hilo lilitolewa katika Ikulu ya Marekani wakati alipokutana na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu. SOMA: Iran kujadili nyuklia na nchi za Ulaya

Trump alifafanua kuwa mazungumzo hayo yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi wiki hii nchini Oman, ambapo Serikali ya Iran imethibitisha kushiriki katika mazungumzo hayo ambayo yatakuwa  ya ndani.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button