DAR-ES-SALAAM: BALOZI wa Marekani nchini Tanzania, Dk. Michael Battle, amezipongeza juhudi za Tanzania katika matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehama) katika kukuza maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Akitangaza washindi watatu wa shindano la US-Tanzania Tech Challenge, Balozi Battle alisisitiza kuwa matumizi ya Tehama sasa ni muhimu, kwani kila kitu kiko mtandaoni.
Balozi Battle aliwataka washindi kutumia ujuzi wao wa Tehama kama fursa na kuwa jukwaa la kuhabarisha umma kuhusu rasilimali zilizopo mtandaoni kwa faida ya taifa.
“Hii ni fursa iliyo mbele yenu, ndoto ambayo nawashawishi muitafute na msikubali kukaribisha ndoto ndogo, na kama una ndoto ndogo basi tafuta mwenye ndoto kubwa ili akushawishi kubuni vitu vipya vya kuabdilisha dunia “, alisema Dk. Battle
Aidha, Dk. Gerald Kafuku, Meneja wa Ubunifu na Teknolojia, aliongeza kuwa serikali inaendelea kuwekeza zaidi katika sekta ya habari na mawasiliano ili kuunga mkono juhudi zinazofanywa na wabunifu chipukizi wa masuala ya Tehama na kufungua ya fursa za kiuchumi.
Alisisitiza kuwa COSTECH inashirikiana na wadau wa maendeleo kuwasaidia wabunifu wachanga katika kuleta mabadiliko chanya katika sekta mbalimbali nchini ili kuliwezesha taifa kusonga mbele.
“lengo la serikali kuibua vipaji vya Tehama hasa ukizngatia ukuaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano inakua kwa kasi sana sasa imekuja akili mnemba lazima tukimbizane nah ii kitu”, Alimalizia Dk. Kafuku
Washiriki zaidi ya 100 walionesha ubinfu wa miradi yao ya Tehama ambapo washindi nane waliingia katika kinyang’anyiro cha kuchaguliwa tatu bora.
SOMA : Samia aikaribisha Marekani uwekezaji maeneo matano
Jamii Forum aliibuka kidedea na kupatiwa $100,000 , mshindi wa pili Smart Foundry alipata $80,000 na mshindi wa tatu Launch Pad Tanzania alipata $70,000.