Marekani, Urusi kumaliza vita Ukraine

RIYADH: VIONGOZI wa Marekani na Urusi walikutana mjini Riyadh, Saudi Arabia, na kukubaliana kuanzisha mchakato wa amani kwa mzozo wa Ukraine, ingawa Kiev na washirika wake wa Ulaya hawakualikwa.

Mazungumzo hayo yaliyodumu kwa masaa manne yalifanyika katika kasri la Diriyah, ambapo pande hizo mbili zilikubaliana kuunda timu ya wapatanishi na kurekebisha mahusiano ya kidiplomasia na kiuchumi.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Marco Rubio, na mwenzake wa Urusi, Sergei Lavrov, walisema majadiliano hayo yalikuwa na manufaa makubwa na ni hatua nzuri ya kwanza.

SOMA: Marekani yasaka amani ya kuduma Ukraine

 

 

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button