Marekani yatiliwa shaka mpango wa nyuklia

URUSI: WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, ametilia shaka nia ya Marekani siku moja kabla ya duru ya pili ya mazungumzo kuhusu mpango wa nyuklia wa Tehran unaotarajiwa kufanyika mjini Rome.
Araghchi aliyasema haya wakati wa mkutano wa waandishi wa habari mjini Moscow akiwa pamoja na mwenzake wa Urusi, Sergei Lavrov, akisisitiza kuwa licha ya mashaka makubwa juu ya nia ya Marekani, watachukua sehemu katika mazungumzo hayo yaliyopangwa kufanyika leo Jumamosi.
Hata hivyo, Waziri huyo wa Mambo ya Nje wa Iran alionyesha matumaini kwamba makubaliano ya nyuklia na Marekani yanaweza kufikiwa kwa msaada wa Urusi, huku Lavrov akisema kuwa Moscw iko tayari kutoa mchango wake kusaidia kuendeleza mpango huo.
Can’t wait to read more posts like this. Subscribed!