Marufuku kuuza chakula nje

RAIS wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amepiga marufu wakulima kuuza mazao nje ya nchi ili kukabiliana na upungufu wa chakula nchini

Rais ametoa agizo   leo June 13, 2023 jijini Mwanza alipokuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha la Utamaduni la Bulabo linaloendelea katika Uwanja wa Red Cross Ngomeni Kisesa jijini humo.

Amesema  tayari amemuagiza Waziri wa Fedha  Mwigulu Nchemba na  Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kuhakikisha wananunua mazao kutoka kwa wakulima msimu huu wa mavuno ili nchi iwe na akiba ya chakula cha kutosha.

“Kwa sasa nchi ina akiba ya chakula tani laki mbili hadi laki mbili na nusu, tunampango wa kumwaga fedha kununua chakula, tunataka kuwa na hifadhi ya chakula  tani laki tano kwa mwaka huu tunaouanza, hivyo msiuze mazao nje kwa kuwa serikali itayanunua.” Amesisitiza Rais Samia.

Habari Zifananazo

Back to top button