Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amemteua Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani na wajumbe wengine 18 akiwemo DCP mstaafu Mohamed Mpinga.
Katika uteuzi huo unaoanza Septemba Mosi, Masauni amemteua Naibu Waziri wa Uchukuzi Atupele Mwakibete, kuwa Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo.
Uteuzi huo ni kwa mujibu wa Kifungu cha 96 ya Sheria ya Usalama Barabarani, Sura ya 168 (The Road Traffic Act, Cap 168).
Wajumbe 18 wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ni pamoja na
1. Dkt. Henry Swai – Mjumbe
2. Ndg. Ponziano Lucian Lukosi – Mjumbe
3. Mhandisi Rogatus .H. Matavila – Mjumbe
4. Mhandisi Victor H. Seff – Mjumbe
5. Rtd DCP Mohamed Mpinga – Mjumbe
6. Ndg. Neema Swai – Mjumbe
7. SACP Johansen Kahatano – Mjumbe
8. Dkt. Baghayo A. Saqware – Mjumbe
9. Mhandisi Yona Africa – Mjumbe
10. Ndg. Isabela Oswald Nchimbi – Mjumbe
11. Ndg. Agustas Fungo – Mjumbe
12. Ndg. Faraji Jaffa Abri – Mjumbe
13. Ndg. Issa Kassim Nkya – Mjumbe
14. Ndg. Dorice John Mutalemwa – Mjumbe
15. Dkt. Ayoub Ryoba – Mjumbe
16. Ndg. Abdallah Miraji – Mjumbe
17. Mhandisi Dkt. Phil Makini – Mjumbe
18. Ndg. Anord Mtewele – Mjumbe