Mashindano ya kriketi kimataifa kuanza leo

DAR-ES-SALAAM: Mashindano ya Cricket World Cup Africa Division 2 Qualifier kuanza  leo katika viwanja vya Gymkhana Posta jijini Dar es Salaam yakishirikisha nchi nane.

Mratibu wa  Mashindano ya Kriketi Tanzania (TCA), Atif Salim amesema katika michuano hiyo kuna timu nane na zimepangwa katika makundi mawili yenye kila kundi timu nne,

“Tanzania ipo kundi  A na Nigeria, Msumbiji na Malawi, huku kundi B likiundwa na Ghana, Botswana, Sierra Leone na Rwanda”, amesema.

Advertisement

Aliongezea kuwa “Washindi wawili wa kila kundi watacheza nusu fainali, kisha fainali  na kutafuta mshindi wa tatu.Watakaocheza fainali tayari wote watakuwa wamefuzu kwenda Division I, na nchi itakayokuwa mshindi wa tatu nayo itafuzu kwenda mbele Division I,” alisema Atif.

SOMA: Majaliwa mgeni rasmi TASWA bonanza

/* */