MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule ameitaka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha kusimamia sheria za michezo hiyo na kuagiza kuondolewa haraka mashine feki ambazo hazilipi kodi kabla ya hatua kuchukuliwa.
DC Mtambule amesema hayo katika semina ya wajumbe wa kamati ya ulinzi iliyofanyika katika ofisi ya yake yenye lengo la kutoa elimu kuhusiana na sheria za michezo hiyo.
SOMA: Leseni mpya 1126 kutolewa michezo ya kubahatisha
Amesisitiza kutekelezwa kwa sheria za michezo hiyo kwa kuhakikisha mashine zinasajiliwa na kupata leseni.
Katika operesheni hiyo, DC Mtambule amekamata mashine 72 zilizokuwa zinafanya kazi kinyume na sheria katika baadhi ya maeneo ya Kinondoni.