Matangazo mtandaoni kutozwa kodi

SERIKALI inatarajia kuanzisha mfumo wa kidijitali wa kufuatilia na kuhakikisha kodi husika za Serikali zinalipwa kwa wakati kwa matangazo ya mitandaoni, hii itajumuisha matangazo ya biashara ambayo huwekwa na watu maarufu (digital influencers) na biashara za mtandaoni zinazofanyika nchini.

Hayo yamesemwa leo June 15,2023 na Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba akiwasilisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 Bungeni jijini Dodoma.

Amesema, kutokana na ukuaji wa teknolojia, dunia inashuhudia mabadiliko makubwa katika tasnia ya matangazo ya kibiashara ambapo sasa matangazo mengi yamekua yakifanyika kupitia mitandao (online advertisement) hasa mitandao ya kijamii kama vile Instagram, Facebook, twitter na Blogs mbalimbali.

Advertisement

“Kwa kushirikiana na sekta binafsi, serikali inatarajia kuanzisha mfumo wa kidijitali wa kufuatilia na kuhakikisha kodi husika za serikali zinalipwa kwa wakati, hii itajumuisha matangazo ya biashara ambayo huwekwa na Watu maarufu (digital influencers) na biashara za mtandaoni zinazofanyika nchini.”Amesisitiza

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *