Mulokozi: Tumeajiri Watanzania 312

DAR ES SALAAM; WATANZANIA 312 wameajiriwa idara mbalimbali katika ya Kampuni ya Mati Super Brands Ltd, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, David Mulokozi amesema.

Akizungumza na HabariLEO, Mulokozi amejivunia kutoa fursa za kazi kwa vijana wasomi na wale wenye ujuzi wa kiufundi.

“Tumeanzisha programu za mafunzo kwa vitendo ambapo vijana wengi wanapata ujuzi na uzoefu unaowasaidia kupata ajira hata nje ya kampuni yetu. Tunatambua kuwa ajira ni changamoto kubwa kwa vijana, na tumejitolea kuchangia katika kupunguza tatizo hili kupitia ajira na mafunzo endelevu,” amesema Mulokozi.

Katika mwendelezo wa kufanya mabonanza na wafanyakazi wa kampuni hiyo, Mulokozi amesema mwaka huu wanatarajia kufanya bonanza kubwa zaidi, ambalo litajumuisha michezo mbalimbali, burudani, na zawadi kwa wafanyakazi waliofanya vizuri zaidi.

“Tunataka kuhakikisha kuwa wafanyakazi wetu wanajisikia kuwa sehemu muhimu ya familia ya kampuni na wanathaminiwa kwa mchango wao,” amesema.

Amesema bonanza hilo ni njia ya kuwashukuru na kuwapa nafasi wafanyakazi kupumzika na kuburudika na kwamba mabonanza hayo yamekuwa yakileta mshikamano na ari ya kazi miongoni mwa wafanyakazi.

Habari Zifananazo

Back to top button