Matukio mbalimbali uzinduzi Ikulu mpya Chamwino

RAIS Samia Suluhu Hassan Kipanda mti wa kumbukumbu kwenye hafla ya ufunguzi wa Jengo la Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma leo Mei 20, 2023.

Rais Samia Suluhu Hassan akitoa hotuba yake mara baada ya kufungua rasmi Jengo la Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma leo Mei 20, 2023.

Rais Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Spika wa Bunge la Tanzania, Dk Tulia Ackson pamoja na Spika wa Baraza la Waakilishi, Zubeir Ally Maulid mara baada ya kufungua Jengo la Ikulu Chamwino mkoani Dodoma leo Mei 20, 2023.

Mwonekano wa jengo jipya la Ikulu ya Chamwino kama linavyoonekana pichani ambalo limezinduliwa rasmi na Rais Samia Suluhu Hassan leo Mei 20, 2023.

Rais Samia Suluhu Hassan akikagua gwaride rasmi la ukaguzi lililoandaliwa na jeshi la polisi mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

Rais Samia Suluhu Hassan akikabidhi Tuzo ya Hayati Rais wa Awamu ya tano Dk John Pombe Magufuli kwa Mama Janeth Magufuli wakati wa sherehe za ufunguzi wa jengo la Ikulu ya Chamwino Dodoma.

Rais Samia Suluhu Hassan akikabidhi tuzo ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa Mama Maria Nyerere wakati wa Sherehe za ufunguzi wa jengo la Ikulu ya Chamwino Dodoma.

Rais Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya kumbukumbu na marais wastaafu Ali Hassan Mwinyi, Dk Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein mara baada ya kuzindua jengo la Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

Rais Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais, Dk Philip Isdor Mpango, Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdalla pamoja na marais wastaafu, Ali Hassan Mwinyi na Jakaya Kikwete wakati akikata utepe kuashiria ufunguzi wa jengo la Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.
