Mavunde ashukuru uanzishwaji shule mpya Kata ya Mpunguzi

Mavunde ashukuru uanzishwaji shule mpya Kata ya Mpunguzi

MBUNGE wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde amemshukuru Rais  Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia madarasa ya uanzishwaji wa shule mbili mpya za msingi na sekondari katika Kata ya Mpunguzi jijini Dodoma.

Mavunde ameyasema hayo leo Desemba 21, 2020 Mpunguzi, wakati wa ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa Shule mpya ya Msingi Mlangwa B na Sekondari mpya ya Nkulabi.

“Mwezi Agosti, 2022 wakati Mheshimiwa Rais amesimama hapa Mpunguzi, tulimuomba madarasa kwa ajili ya uanzishwaji wa Shule mpya za Msingi Mlangwa B na Sekondari Nkulabi, ili kuwapunguzia mwendo watoto hawa wa shule ambao wanatembea Kilometa 9 kufuata shule,”amesema Mavunde na kuongeza:

Advertisement

“Tunamshukuru Mheshimiwa Rais kwa kulipokea ombi letu na sasa utekelezaji umeanza rasmi,” amesema na kuwashukuru  wananchi wa maeneo hayo  kujitolea nguvu kazi katika mradi mradi huo.

“Rai yangu kwa wataalamu wetu ni kuhakikisha mnasimamia vizuri ujenzi wa shule hizi kwa ubora wa hali ya juu na mradi ukamilike kwa wakati, ili mapema Januari 9, 2023 watoto waanze kuyatumia haya majengo,” amesema Mavunde.

Akitoa maelezo ya awali Diwani wa Kata ya Mpunguzi, Innocent Nyambuya, amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapunguzia mwendo watoto wa Mpunguzi kupitia ujenzi wa shule hizo.

2 comments

Comments are closed.

/* */