Mayele ampongeza Saido

JANA mshambuliaji wa Simba ya Dar es Salaam, Saido Ntibazonkiza alianza kwa kishindo kuichezea timu hiyo akifunga mabao matatu katika ushindi wa mabao 7-1, ambao Simba iliupata dhidi ya Prisons.

Mara moja baada ya kuona kiwango cha Saido katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele amesema Saido anastahili pongezi.

Kupitia Akaunti yake ya Instagram Mayele ameandika: “Hongera sana Saido, mchezaji mkubwa ni mkubwa.”

Kwa upande wake Saido ambaye huo ulikuwa mchezo wake wa kwanza tangu ajiunge na Simba amesema anapambana kuhakikisha anasaidiana na wenzake kufikia malengo ya timu hiyo ifikapo mwishoni mwa msimu na anajisikia mwenye furaha kuanza vizuri kibarua chake kipya, akiwa na timu kubwa Simba.

Licha ya mabao hayo, Saido alihusika na bao moja lililofungwa na John Bocco ambaye naye alifunga mabao matatu katika mchezo huo.

Habari Zifananazo

Back to top button