Mayele: Ni msimu wangu bora maishani

Mayele

MSHAMBULIAJI waYanga, Fiston Mayele amesema anajivunia kuhusika kwenye mafanikio ya timu yake ya Yanga katika michuano mbalimbali, huku akikiri kuwa huu ndio msimu bora zaidi kwake katika maisha yake ya soka.

Akizungumza baada ya mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) kati ya Singida Big Stars na Yanga uliomalizika jioni hii mkoani Singida na yeye kufunga bao pekee katika mchezo huo, hivyo kuipeleka Yanga hatua ya fainali, amesema msimu huu umekuwa wa mafanikio kwake katika michuano ya kitaifa na kimataifa.

“Nmeshiriki michuano ya CAF (Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika), mara nyingi lakini sikuwahi kufunga mabao saba au sita, nilikuwa ninafunga, lakini mabao matatu au mawili kwa hiyo nina furaha sana na msimu huu,” alisema Mayele.

Advertisement

Mayele anaongoza katika ufungaji Ligi Kuu Tanzania Bara akiwa na mabao 16, lakini pia ana mabao sita katika Kombe la Shirikisho Afrika ambapo Yanga imeingia hatua ya fainali.

1 comments

Comments are closed.