Mazungumzo ya amani DRC, Rwanda yaendelea Doha

DOHA: MJUMBE Maalum wa Rais wa Marekani, Donald Trump, kuhusu masuala ya Afrika, Massad Boulos, amekutana leo mjini Doha na wawakilishi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Rwanda, katika juhudi za kutafuta suluhu ya mgogoro mashariki mwa DRC.
Mkutano huo umefanyika kufuatia makubaliano ya awali ya pande hizo mbili kuanza mazungumzo ya amani, huku Boulos akieleza kupitia mtandao wa X kuwa pia amekutana na maafisa wa Ufaransa, Qatar na Togo nchi inayowakilisha Umoja wa Afrika kama mpatanishi wa mgogoro huo.
Boulos amesema lengo kuu la mkutano huo ni kuendeleza dhamira ya pamoja ya kuleta amani, utulivu na ustawi katika eneo la maziwa makuu, ambalo limeendelea kukumbwa na migogoro ya mara kwa mara.
Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar, mazungumzo hayo yamegusia kwa kina mgogoro wa mashariki mwa DRC, hali ya kibinadamu na umuhimu wa mwitikio wa haraka wa kimataifa katika kusaidia raia walioathiriwa.
SOMA: Tshisekedi , Kagame wakubaliana kuyamaliza mapigano
Qatar imeelezwa kuendelea kuwa mpatanishi muhimu katika mzozo huo ambao umesababisha maelfu ya watu kupoteza makazi katika miezi ya hivi karibuni kutokana na mapigano ya vikundi hasimu mashariki mwa DRC.
buy viagra online