Mbosso amshukuru Kikwete kwa matibabu

MSANII wa muziki wa bongo fleva Mbwana Kilungi ‘Mbosso’ amemshukuru Rais wa awamu ya nne Dk Jakaya Kikwete kwa kupona matatizo ya moyo.

Hata hivyo, Kikwete alisema yeye hastahili hizo pongezi alitoa wazo tu la kujengwa kwa Kituo Cha matibabu ya Moyo hivyo wanaopaswa shukrani hizo ni JKCI na Rais Samia Suluhu Hassan.

Mbosso alikutana na Kikwete juzi Dar es Salaam na kusema amefurahi kuona msanii huyo amepona na kuahidi atamsaidia kumkutanisha na Rais Samia ili kumpa shukrani kwa juhudi kubwa za kuboresha sekta ya afya nchini.

Advertisement

Kupitia akaunti ya Mbosso ya mtandao wa Kijamii aliweka video ikimuonesha kwenye mazungumzo na Rais huyo mstaafu na kusema:

“Nimepata nafasi ya kumtembelea mheshimiwa Jakaya kikwete, Rais wa awamu ya nne wa Tanzania, nyumbani kwake ili kutoa shukrani zangu za dhati kwa matibabu niliyopata kupitia taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na pia kuwasilisha shukrani zangu kwa Dk Peter Kisenge Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI,” alisema Mbosso.

Aliongeza: “Mbali na hayo Dk Kikwete ameniahidi atasaidia nipate fursa ya kumshukuru Rais Samia kwa juhudi zake kubwa katika kuboresha sekta ya afya nchini Tanzania Mungu awabariki wote wanaojitolea kuokoa maisha.”

 

Dk Kikwete alitoa rai kwa watu kujenga utamaduni wa kuangalia afya zao na kuchukua hatua mapema.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *