Mbosso kunogesha kampeni za Manara Kariakoo leo

DAR ES SALAAM : MSANII maarufu wa muziki wa kizazi kipya, Mbwana Kilungi ‘Mbosso’ leo Oktoba 27, 2025, anatarajia kunogesha ufungaji wa kampeni wa mgombea udiwani wa Kata ya Kariakoo, Haji Manara.

Akizungumza na Daily News Digital, Manara amesema mkutano wa kufunga kampeni utafanyika makutano ya mitaa ya Msimbazi na Jangwani, Dar es Salaam na kwamba wadau mbalimbali watakuwepo.

Amewataja baadhi ya waalikwa wengine maarufu ni Waziri wa Mifugo, Abdallah Ulega, Naibu Spika, Mussa Azzan ‘Zungu’ na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoaw wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu  kusisitiza kuwa mkutano huo utakuwa wa aina yake.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button