Mbunge afanikisha ujenzi jengo la wajawazito

MBUNGE wa Jimbo la Buhigwe Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, Felix Kavejuru amekabidhi mabati 87 kwa zahanati ya kijiji cha Nyakimwe ili kukamilisha jengo la kujifungulia wajawazito baada ya jengo hilo kukaa muda mrefu bila kukamilika.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye eneo la sokoni la kijiji hicho, sambamba na kukabidhi idadi hiyo ya mabati, pia mbunge huyo ameahidi kugharamia mbao zote za kenchi kwa ajili ya kuezekea, mifuko 20 ya sementi, misumari na gharama za ufundi zinatakazowezesha kukamilika kwa jengo.

Mbunge wa Buhigwe, Felix Kavejuru akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Nyakimwe wilayani Buhigwe baada ya kukabidhi mabati kwa serikali ya kijiji ili kukamilisha ujenzi wa chumba cha kujifungulia wajawazito katika zahanati ya kijiji hicho
Katika mkutano huo wa hadhara mbunge huyo amesema kuwa alipokea maombi ya ya uongozi wa zahanati na kijiji wakiomba asaidie kukamilisha jengo hilo ambapo aliahidi kusaidia ujenzi huo na kwamba umefika wakati wa kutimiza ahadi yake ili kuhakikisha utoaji huduma katika jengo hilo la kujifungulia kina mama linakamilika.

Wananchi wa kijiji cha Nyakimwe waliohudhuria mkutano wa mbunge, Felix Kavejuru.
Baadhi ya wananchi wa kijiji akiwemo akiwemo Evetha Marco ambaye amejifungua mtoto wake katika zahanati hiyo alisema kuwa kwa sasa ni usumbufu mkubwa kwani kuna chumba kimoja na kitanda kimoja kinachotumika hivyo baada ya kujifungua alilazimika kutoka ili kumpisha mama mwingine ambaye naye alishafika muda wa kujifungua.
Kufuatia msaada huo uliotolewa na mbunge mwananchi mwingine wa kijiji hicho, Neema Robert amesema kuwa wanafarijika kuona hitaji lao sasa linakwenda kukamilika kwani chumba jengo hilo la kujifungua kina mama limekaa muda mrefu na sasa linakwenda kukamilika.

Viongozi wa serikali ya kijiji cha Nyakimwe waliohudhuria mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Buhigwe, Felix Kavejuru.
Mganga Mfawidhi wa zahanati hiyo, Ruben Mbuya amesema kuwa kukamilika kwa jengo hilo la kujifungulia kuna mama kutawapa nafasi nzuri ya kutoa huduma kwani kwa sasa wanatumia moja ya vyumba vya zahanati hiyo ambacho hakikidhi mahitaji.

Neema Robert mwananchi wa kijiji cha Nyakimwe ambaye amejifungulia kwenye zahanati ya kijiji hicho.



