Mbunge ataka wananchi wapewe nyama ya tembo wale

DODOMA; MBUNGE wa Viti Maalum, Dk Thea Ntara, amesema ni kama serikali inafikiria kupunguza wanyama wakorofi wakiwemo tembo wanaovamia makazi ya watu ni vyema wakawaua, kisha nyama yake wapewe wananchi katika mikoa ambayo wanakula nyama hiyo ikiwemo Mkoa wa Ruvuma.

Akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka wa fedha 2024/24, Mbunge Ntara amesema tembo wamekuwa wakisumbua wananchi kwa kuvamia maeneo ya watu, lakini kwa vile yapo maeneo watu wanakula nyama yake ikiwemo mkoani Ruvuma ni vyema sasa Serikali ikafikiria utaratibu wa kuua wanyama wakorofi , kisha nyama yake wakapatiwa wananchi.

Isome pia:https:https://habarileo.co.tz/malipo-madhara-wanyamapori-yaongezwa/

”Lakini pia Mheshimiwa Waziri, suala la tembo, Ruvuma tunakula sana nyama ya tembo. Hebu niwaombe kama mnafikiria kupunguza, muwachinje sijui niseme kuwaua, halafu tengenezeni hizo nyama, pelekeni mikoa ambayo tembo wanaliwa.

“…Mjipange kuhusu hawa wanyama wanaoua wapunguzeni, sisi tupo tayari kula hiyo nyama,” amesema Mbunge huyo.

 

Habari Zifananazo

Back to top button