Mbunge EALA ataka mabadiliko ya lugha bungeni

MBUNGE wa Bunge la Afrika Mashariki ( EALA ) kutoka nchini DR Congo, Masirika Dorothee amesema mabadaliko ya sheria mbalimbali katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ni muhimu katika kuwezesha baadhi ya wabunge wa bunge hilo kununua vifaa ili kuwezesha wabunge wasiojua Kiswahili wala Kifaransa kutambua kinachoendelea ndani ya bunge.

Amesema ni lazima mikataba hiyo itambulike na kuwezesha lugha hizo ikiwemo Kingereza kutumika ili kuwezesha wabunge wengi kuchangia mada mbalimbali ili wananchi waweze kuelewa kinachoendelea.

Amesema sheria zisizotekelezeka zilizotungwa na Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) zinakwamisha baadhi ya mambo mbalimbali kutotekelezeka kwa wakati.

Aidha ununuzi wa vifaa vya kutafsiri lugha ni muhimu kwa baadhi ya wabunge lakini bado ni changamoto ya kuvinunua sababu ya baadhi ya sheria hazijarekebishwa za kuwezesha lugha ya Kifaransa na Kiswahili kutumika kama lugha rasmi ndani EAC.

Awali akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo katika bunge hilo, Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria, Haki na Ardhi, Mashaka Ngole ametoa rai kwa Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Peter Mathuki kuangalia sheria zinazotakiwa kufanyiwa marekebisho ili kuwezesha baadhi ya mikataba kurekebishwa sanjari na lugha hizo na kingereza kuweza kutumika.

Kwa mujibu wa Ngole kamati hivyo imefanya ziara kwenye taasisi za EAC katika nchi mbalimbali na kubaini kuwa zinashindwa kutekelezwa majukumu yake kutokana na sheria na baadhi ya vipengele kwenye mkataba wa uanziahwaji wa nchi za EAC kutofanyiwa marekebisho licha ya wakuu wa nchi wanachama kuelekeza marebisho Hayo kufanyika.

“Wajumbe wa kamati hii wametembelea taasisi zote zinasimamiwa na EAC katika nchi mbalimbali wanachama na kuona changamoto zinazowakabili watumishi wa taasisi hizo. Hivyo tunatoa rai kwa nchi hazijatoa ardhi zilizoahidi kwa akili ya ujenzi wa ofisi za Taasisi hivyo watoe ili ujenzi uweze kuanza wa majengo ya kudumu”

Habari Zifananazo

Back to top button