RAIS Samia Suluhu Hassan amemteua Nehemia Mchechu kuwa Msajili wa Hazina kuanzia leo Februari 24, 2023, kabla ya uteuzi huo Mchechu alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus, imesema Mchechu anachukua nafasi ya Mgonya Benedicto ambaye atapangiwa majukumu mengine.
Taarifa imesema Rais Samia amemteua Hamad Abdallah kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC kuanzia leo Februari 24, 2023, akichukua nafasi ya Nehemia Mchechu ambaye ameteuliwa kuwa Msajili wa Hazina.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Rais Samia pia amemteua Mussa Mohammed Makame kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania (TPDC), akichukua nafasi ya James Mataragio ambaye atapangiwa majukumu mengine.