Mchengerwa: Wakurugenzi jengeni vituo vya bodaboda

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mohamed Mchengerwa amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kuhakikisha wanajenga vituo vya bodaboda vya kuegesha pikipiki vyenye uwezo wa kuzuia jua na kuwakinga na mvua.

Mchengerwa ametoa maelekezo hayo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salam, wakati akizindua sare maalum na mfumo wa kidijitali (kanzidata) wa madereva bodaboda na bajaji wa jiji hilo.

“Ninaelekeza vituo hivi vijengwe mara moja ili kuwasaidia bodaboda kupata eneo salama la kupaki wakati wakisubiria wateja,” Mchengerwa amesisitiza.

Sanjari na hilo, Mchengerwa amewaelekeza Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kuanza mchakato wa kutoa mikopo ya asilimia 10 kwa wanawake, vijana na wenye ulemavu mara moja ndani ya mwezi huu ili walengwa wanufaike na mikopo hiyo kama ilivyokusudiwa na Serikali.

Habari Zifananazo

Back to top button