Mchungaji apongeza Lugumi kuwajenga ghorofa yatima

KITENDO cha mfanyabiashara Said Lugumi kuwajengea nyumba ya ghorofa watoto yatima kimewagusa baadhi ya waumini wa dini mbalimbali nchini, huku baadhi yao wakipongeza hatua hiyo.

Desemba 25, akizungumza na waandishi wa habari, Lugumi alikabidhi majengo saba ya ghorofa 4 kwa ajili ya kulea watoto zaidi ya 800 waliopo Mkoa wa Dar es salaam ikiwa ni katika kusaidia kundi hilo ambalo linahitaji makazi ya pamoja na malezi.

Mchungaji wa Kanisa la Miracle International, Daniel Julius akiwa katika madhabau ya kanisa hilo amempongeza mfanyabiashara Said Lugumi kwa kuwajengea watoto yatima maghorofa kwa ajili ya makazi na kuwalea kama watoto wake.
A
“Huyu Lugumi ameishia darasa la saba kama anavyosema lakini amewajengea yatima ghorofa tano na kila ghorofa wanatakiwa kuishi yatima 100 kwenye makazi hayo, je huyu mtu hatapata swawabu kutoka kwa Mungu ambaye anawaangalia yatima,”?

“Atapata swawabu kwa sababu amewaangalia wale waliokuwa hawawezi, yule Lugumi si muislamu na amewatendea yatima mema, kama dini yako haikuzuii kutenda mabaya’ inakuacha unatenda mabaya na dini ya mwingine unayoiona haifai inamruhusu kutenda mema dini iliyo njema ni ipi,” amehoji mchungaji Daniel.

“Yeye anawatendea mema wale ambao hata sio ndugu zake, hawajui kabisa, fanyeni mema kama maandiko yanavyosema tusichoke kutenda mema maana katika kutenda mema hatutazimia mioyo, sasa anawalisha watu ambao yawezekana wazazi wao walikuwa ni watu wenye tabia tofauti lakini yeye amefika mahali kwa kuwajengea maghorofa matano unafikiri wale yatima wanapomuangalia, wanamwambia Mungu tunashukuru, si sifa zinarudi kwa Mungu, Mungu nae anangalia Lugumi uko wapi njoo nikuongezee kingine,” ameongeza.

Habari Zifananazo

Back to top button