MELI ya Sea Ruby imetia nanga katika Bandari ya Mtwara kwa ajili ya kushusha salpha kwa ajili ya kupulizia mikorosho katika mikoa ya Lindi, Ruvuma na Mtwara.
Meli hiyo imewasili katika Bandari ya Mtwara Mei 25, 2023 ikiwa imebeba salpha tani 3,680 ikitoka Misri kupitia Mombasa.
Akizungumza leo na waandishi wa habari Mkoani hapa, Meneja wa Bandari ya Mtwara Norbert Kailembo, amesema meli hiyo inatarajia kuondoka kesho baada ya kumaliza kushusha hiyo salpha.
“Meli ya Sea Ruby imefika tarehe 25 Mwezi huu wa tano, ikiwa imebeba tani 3680 za salpha kwa ajili ya kupulizia mikorosho, meli imetoka Misri ikapitia Mombasa na kuja hapa (Bandari ya Mtwara),” amesema.