AFRIKA YA KUSINI: Wimbo wa taifa wa Tanzania “Mungu ibariki Afrika” ulibuniwa na mtunzi kutoka Afrika Kusini Enoch Sontonga.
SOMA:https://habarileo.co.tz/wimbo-wa-taifa/
Wimbo huu asili yake ni wimbo Nkosi Sikelel’i Afrika aliotunga mwaka 1897.
Tafsiri ya jina hilo kwa kiswahili ni Mungu Ibariki Afrika.
Ni wimbo maarufu zaidi Afrika ukitumika pia katika harakati za ukombozi kwa baadhi ya nchi za Afrika.
SOMA:https://www.bbc.co.uk/programmes/b06qjtqs
Maneno ya wimbo huo pia yanatumika kwenye nyimbo za taifa kwa nchi za Afrika Kusini,Zambia na Zimbabwe.
Sontonga alizaliwa mwaka 1873 na kufariki 18/04/1905.
Kila mtu hukumbukwa duniani kwa alama aliyo iacha