Mfaume ataka pambano la Oscar, Tony lirudiwe

NAHODHA wa Nàccoz Gym, bondia wa ngumi za kulipwa Mfaume Mfaume ameomba pambano la Oscar Richard na Tony Rashid lirudiwe kutafuta uhalali wa mshindi.

Kwa mujibu wa Mfaume, mpaka leo hawaamini bondia wao Oscar alipigwaje na Tony kwa kuwa ni mtu mwenye uwezo kuliko mpinzani wake.

SOMA: Ishu ya pambano la Mwakinyo kuyeyuka ipo hivi

Katika pambano lililofanyika Juni mwaka huu Oscar aliyeko chini ya Nakoz Gym alipigwa kwa pointi hivyo, wanatamani liandaliwe pambano lingine kulipiza kisasi.

Akizungumza na Dailynews Digital Mfaume amesema:”Muda wowote, saa yoyote tunahitaji pambano na yule jamaa yaani Tony Rashid tukapoteza kwa pointi.

“Tunakubali kwamba katika michezo siku zote kuna kushinda, kutoka sare na kupoteza, tunaheshimu maamuzi ya majaji. Kama majaji walimpa ushindi yule tunaomba mechi ya marudiano tuko tayari,”amesema.

Amesema hata kama ni kesho wanaamini bondia wao Oscar anaweza kushinda kutokana na kuimarika na kuwahakikishia mashabiki wa ngumi kuwa Tony hatomaliza pambano hilo.

Habari Zifananazo

Back to top button