MKUU wa wilaya ya Kilindi Hashim Mgandilwa amewataka viongozi wa dini wilayani humo kuwa makini na wageni wanatumia nyumba za ibada kama gesti huku baadhi wakiwa wanajihusisha na vitendo viovu vya uhalifu.
Ametoa rai hiyo leo Septemba 8, 2023 katika ibada ya swala ya Ijumaa kwenye msikiti wa Taq’wa uliopo katika eneo la Bokwa Kwastemba wilayani Kilindi.
Amesema, licha ya lengo zuri la kuwasaidia wasafiri na wageni kama ambavyo vitabu vya dini vinaelekeza lakini kutokana na nyakati kubadilika ni muhimu kuwa makini na wageni ambao wanalala katika nyumba hizo.
“Niwaombe viongozi wa dini kuwa makini na wageni wanaofika kwenye maeneo yenu na kuwahifadhi kwenye misikiti kama nyumba za kulala wageni.”Amesema
Amesema, baadhi ya wageni wanafanya vitendo vya uhalifu mitaani na kukimbilia kujificha kwenye nyumba hizo.
Comments are closed.