Mganga mkuu Ubungo aagizwa kukagua zahanati Msingwa

MGANGA Mkuu wa Manispaa ya Ubungo mkoani Dar es Salaam, Tulitweni Mwinuka ameagizwa kwenda kukagua Zahanati ya Msingwa iliyopo kata ya Msigani na kueleza huduma zinaanza lini.

Agizo hilo limetolewa na Meya wa Manispaa hiyo, Jaffary Nyaigesha katika Kikao cha robo ya pili katika Mkutano wa Baraza la madiwani, unaojadili taarifa za robo ya pili inayoishia Desemba.

“Mimi binafsi nina maslahi katika zahanati hiyo. Kesho ( leo) uende. Nakuagiza kesho (leo) asubuhi uende ujue imefikia wapi,”.

Awali Mwinuka alisema jengo la kutolea huduma limekamilika, ila choo bado.

Alisema imani yake katika robo inayoendelea itakuwa imekamilika na kuanza kutoa huduma kwani hivi sasa inahudumia wagonjwa wa nje.

Katika hilo Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Ubungo, Elias Ntiruhungwa amesema, zahanati hiyo itaanza Februari 15, mwaka huu.

Habari Zifananazo

Back to top button