Watu 25 wapoteza maisha Pakistan

PAKISTAN : WATU wapatao 25 wameuliwa kati ya waumini Wakiislam wa madhehebu ya Shia na Sunni waliojihami na silaha kuhusiana na mgogoro wa ardhi kaskazini magharibi mwa Pakistan.

Mapigano hayo yaliyoanza mwishoni mwa wiki hii katika wilaya ya Kurram, mkoa wa kaskazini magharibi wa Khyber Pakhtunkhwa unaopakana na Afghanistan, yaliendelea jana Jumatano.

Msemaji wa serikali ya jimbo Barrister Saif Ali, amesema mamlaka wakisaidiwa na wazee wa makabila wanajaribu kutuliza hali ya wasiwasi na pande zote zimekubali kufanya mazungumzo ya amani kufuatia mazungumzo yaliyofanyika Kurram.

 SOMA : Mlipuko wauwa watu 57 Pakistan

 

Habari Zifananazo

Back to top button