MTU mmoja amegundulika kuwa na ugonjwa wa mpox kwenye gereza la Nakasongola katika ya Uganda.
Msemaji wa Idara ya Magereza Uganda Frank Baine amesema mgonjwa huyo ametengwa na anapatiwa matitabu.
Agosti mwaka huu Shirika la Afya Duniani(WHO) lilitangaza mpox kuwa tatizo la dharura duniani kwa mara ya pili katika muda wa miaka miaka kufuatia mlipuko wa virusi vya ugonjwa huo katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ambao umesambaa nchi kadhaa zikiwemo Burundi, Uganda na Rwanda.
SOMA: Tanzania kudhibiti Mpox
“Kwa bahati mbaya mgonjwa hajapata dhamana kwa sababu anashikiliwa kwa tuhuma za mauaji. Tunahisi amekuja na ugonjwa huo gerezani lakini hilo linachunguzwa,” amesema Baine.
Mpox inaweza kuenea kupitia kugasana. Kwa kawaida ni ugonjwa wa wastani, lakini kwa nadra unaweza kusababisha kifo. Kawaida husababisha dalili kama za mafua na vipele vyenye usaha kwenye mwili.