Mhadhiri Chuo Kikuu Mzumbe agongwa, afa

MHADHIRI Kitivo cha Sheria Chuo Kikuu Mzumbe, Ndaki ya Mbeya, Yollana Seme amekufa baada ya kugongwa na lori.

Taarifa ya Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko Chuo Kikuu cha Mzumbe, Rose Mdami imeeleza kuwa Seme aligongwa jana katika eneo la Mbembela – Simike, akiwa njiani kwenda kazini.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Seme aliajiriwa na Chuo Kikuu Mzumbe mwaka 2003 akiwa Mkufunzi Msaidizi katika kitivo cha sheria na alijiendeleza kielimu kwa nyakati tofauti, hadi kufikia cheo cha mhadhiri.

“Hadi umauti unamkuta marehemu Seme, alikuwa katika hutua za mwisho za kuhitimisha masomo yake ngazi ya Shahada ya Uzamivu (PhD), Chuo Kikuu cha Kikatoliki, Ruaha,” alieleza Rose.

Taarifa ilieleza kuwa Seme mbali na kufundisha, pia ameshiriki katika shughuli za utafiti katika masuala ya sheria za kazi na kuwa mjumbe katika Kamati ya Mabadiliko ya sheria chini ya Wizara ya Kazi, Maendeleo ya Vijana na Michezo na aliandika makala za kitaaluma.

 

Habari Zifananazo

Back to top button