Mhagama awajulia hali majeruhi kuporomoka jengo

WAZIRI wa Afya Jenista Mhagama leo Novemba 20 amewajulia hali majeruhi watatu wa ajali ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa iliyotokea Kariakoo, Dar es Salaam Novemba 16, ambao wamelazwa katika Taasisi ya Mifupa- MOI wakiendelea na matibabu akiwemo mwanafunzi wa kidato cha nne. Waziri Mhagama amewatembelea majeruhi hao akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Ismail Rumatila pamoja na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu (hawapo pichani).