Waaswa kukomesha migogoro wachimbaji wadogo, wawekezaji

Waaswa kukomesha migogoro wachimbaji wadogo, wawekezaji

WAZIRI wa Madini, Dk Doto Biteko, amewaasa wanajiolojia kuacha tabia ya kuleta migogoro, baina ya wawekezaji na wachimbaji wadogo wa madini haswa katika leseni na kuiletea serikali hasara kutokana na tamaa za fedha.

Dk Biteko ameyasema hayo leo jijini Arusha, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Jumuiya ya Wanajiolojia Tanzania(TGS) unaofanyika jijini Arusha.

Pia serikali ipo hatua za mwisho za kukamilisha kuundwa kwa  bodi ya usajili ya wanajiolojia hao, ili kuondoa taswira ya ukanjanja katika fani hiyo yenye heshima nchini.

Advertisement

Amesema migogoro mingi iliyopo haswa kwa wachimbaji wa madini imesababishwa na wanajiolojia baadhi, wasio waaminifu, ambao wanasababisha wachimbaji wadogo kuilaumu serikali, wakati matatizo hayo yamesababishwa na wanajiolojia hao.

” Wanajiolojia mnasababisha migogoro kwa wachimbaji wadogo au wawekezaji kwa maslahi yenu,  ukifuatilia zaidi unagundua kuwa waliosababisha migogoro hii ni nyie wataalam kwa maslahi yenu, “ amesema.