Mikoa minne kunufaika kambi ya kibingwa ya matibabu

WATU zaidi ya 300 kutoka Mikoa minne ya kanda ya kaskazini ya Arusha ,Kilimanjaro,Tanga na Manyara wanatarajia kunufaika na kambi ya siku tatu ya matibabu ya kibingwa Jijini Arusha kwa magonjwa ya Moyo,Ubongo na Mgongo kutoka kwa Madaktari Bingwa kutoka Califonia Marekani na wa hapa nchini.
Kambi hiyo ambayo itaongozwa na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo na Mishipa ya Damu kutoka Califonia- Marekani ,Dk Manuf Shamji akishirikiana na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Kichwa ,Ubongo,Mgongo na Mishipa ya Fahamu wa hapa nchini Dkt Clement Mugisha wa Hospital ya Aga Khan wataanza kambi hiyo aprill 27 mwaka huu hadi mei mosi mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Meneja na Mratibu wa Tanlink Medical Tourism Agency,Baraka Farles alisema Hospital ya Aga Khan ya hapa nchini na Heart Medical Group kutoka Califonia Marekani kwa pamoja wanatarajia kutoa huduma hiyo ya tiba kwa idadi hiyo katika kambi ya uchunguzi na matibabu ya kibingwa na bobezi kwa magonjwa hayo katika Hospital ya Aga Khan ya Jijini Arusha kuanzia aprill 27 mwaka huu hadi mei mosi mwaka huu.
Farles alisema na kuwaomba watanzania kuchangamkia fursa hiyo adhimu kwa jitokeza kwa wingi katika kambi hiyo ya siku tatu yenye madaktari bingwa wa magonjwa hayo kutoka nchini Marekani na kwa kushirikiana na Madaktari Bingwa wa hapa nchini kwani fursa hiyo ni mkombozi kwao kwa kupata uchunguzi na tiba kwa bei elekezi na kwa wale wenye Bima ya Afya watapata huduma hiyo pasipokuwa na shaka yoyote.
Meneja na Mratibu wa kambi hiyo alisema uamuzi wa kuchukuwa madaktari bingwa wa magonjwa hayo kutoka nje ya nchi kwa kushirikiana na wa hapa nchini ni kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan za kusogeza huduma ya afya kwa jamii kwa wenye uhitaji wa tiba kwa magonjwa hayo makubwa ambayo kwa kiasi kikubwa yana gharama kubwa na upatikanaji wa tiba yake ni changamoto.
Naye Dkt Vaneshwar Ashok wa Hospital ya Aga Khan Arusha alisema kuwa kambi ya matibabu ya kibingwa na bobezi ni muhimu sana kwa afya na jamii kwa ujumla kwa sababu ya ongezeko kubwa la magonjwa ya moyo,uti wa mgongo na mgongo hapa nchini Tanzania na inakadiriwa kuwa asilimia 25 hadi 40 ya watu wazima hapa nchini wanashinikizo la damu lakini wengi hawajui hali zao.
Dkt Ashok alisema shinikizo la damu isipo gundulika mapema linaweza kusababisha madhara makubwa kama kiharusi ,shambulio la moyo,moyo kushindwa kufanya kazi ,figo kuharibika na hata kusababisha kifo cha ghafla hivyo aliwaasa wananchi wa Mikoa hiyo kujitokeza kwa wingi katika kambi hiyo ya siku tatu lengo likiwa moja kujua afya kwa ujumla.
Alisema Tanzania ina bahati kubwa sana kwa ujio wa daktari bingwa wa magonjwa hayo kutoka Califonia Marekani kuja hapa nchini kutoa huduma ya magonjwa hayo kwa kushirikiana na madaktari wa hapa nchini na kuwataka watanzania kutumia fursa hiyo kikamilifu bila kuchelewa kwani baadae wanaweza kuijutia.




https://shorturl.fm/Us9Q6