NAIBU Waziri wa Madini, Dk Steven Kiruswa amesema mkakati wa wizara hiyo ni kuhakikisha taasisi zake zinaelekeza nguvu katika mikoa yenye madini ya kimkakati ikiwemo kufanyiwa utafiti wa kina wa haraka ili kufikia asilimia 50 kabla ya mwaka 2030.
Aidha amesema mkakati wa wizara hiyo ni kupitia Dira 2030, yenye kauli mbiu ya madini ni maisha na utajiri itawezesha vijana wanaochimba madini kujikwamua kiuchumi ikiwemo kuendelea kufanya utafiti kutoka asilimia 16 iliyopo sasa na kufikia asilimia 50 ifikapo mwaka huo.
Hayo yamesemwa leo Arusha na Naibu Waziri wa Madini, Dk, Kiruswa wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizaraya Madini
Amesema utafiti wa kina wa madini ukifanyika utawezesha ongezeko la fedha ikiwemo serikali kupata mapato sanjari na vijana wanaochimba madini kujikwamua kiuchumi kupitia sekta hiyo.
Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini,Msafiri Mbibo amesema katika kipindi cha kuanzia Julai 2024 hadi Februari, 2025 wizara hiyo imepata mafanikio mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuimarika kwa mchango wa sekta ya madini katika Pato la Taifa na kufikia asilimia 9.0 mwaka 2023 na kasi ya ukuaji kufikia asilimia 11.3 mwaka 2023
Sakarya Elit Escort Kızlarla Vip Bayanlar Esort Güzel Vakit Geçirin
Sakarya Elit Escort Kızlarla Vip Bayanlar Esort Güzel Vakit Geçirin