Mikoko 6,000 yapandwa Pwani ya Miseti

KATIKA kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani, wadau kwa kushirikiana na wananchi pamoja na viongozi wa serikali mkoani Mtwara wamepanda mikoko 6,000 na usafi wa mazingira katika Pwani ya Miseti kata ya Chuno Manispaa ya Mtwara Mikindani.

Zoezi hilo limeongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Abdallah Mwaipaya leo Mei 31, 2025 kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala.

Aidha lengo la zoezi hilo ikiwa ni pamoja na kuendelea kulinda mazingira ya bahari na kuzuia mmomonyoko wa udongo ambapo huko nyuma kupitia zoezi hilo wamefanikiwa kupanda mikoko zaidi ya 30,000 katika Pwani hiyo.

Mkuu huyo wa wilaya, amevitaka vikundi na vilabu vya mbio kushirikiana na wananchi kuweka utamaduni wa kufanya usafi wa pamoja kila ifikapo jumamosi ya mwisho wa mwezi ili kuendelea kuuweka mkoa huo katika mazingira masafi.

“Tukiwa na mazingira machafu tunajiweka katika hatari ya kupata maradhi ya mlipuko pia tunatengeneza mazalia ya mbu ambao wanasababisha ugonjwa mkubwa wa malaria, tusafishe mazingira yetu ili tuwe salama wakati wote,” amesema Mwaipaya

Baadhi ya washiriki wa zoezi hilo akiwemo Katibu wa kikundi cha miseti women group Melesiana Adolf amepongeza umoja huo na kuendelea kutoa hamasa kwa wananchi kuwa zoezi hilo liwe endelevu kwa maslahi mapana ya mkoa huo.

Maadhimisho hayo yanaenda na kauli mbiu inayosena ” Mazingira Yetu na Tanzania ijayo Tuwajibike sasa, Dhibiti Natumizi ya Plastiki.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button