Active Mama: Mikutano kimataifa itumike kujitangaza

MKURUGENZI wa Taasisi ya Active Mama, Ernestina Mwenda amewataka watanzania kutumia mikutano ya kimataifa inayofanyika hapa nchini katika kujitangaza katika soko la kimataifa.

Akizungumza na mwandishi wa Habari Leo, alisema Tanzania imekuwa ikipokea mikutano mikubwa kama Mkutano wa kimataifa wa Chakula uliofanyika Dar es Salaam na kukutanisha viongozi wakubwa  kutoka nchi mbalimbali za Afrika.

Alisema kampuni yake ya Active Mama,  imejipanga kutumia fulsa hizo zinazotokana na mikutano hiyo katika kupeleka bidhaa zake katika soko la kimataifa hasa katika upande wa Afrika Mashariki na Kati.

“Soko ni la kulipambania hivyo zinapotokea fulsa kama hizi za mikutano mikubwa, ni muda sahihi wa kuhakikisha bidhaa za ndani na kuhakikisha  zinasambaa” alisema.

Ernestina alisema anaamini bidhaa zake na za Tanzania, zinanafasi kubwa katika soko la kimataifa kwakuwa za asili na zinapendwa kutokana na  hlkutokuwa na vimelea vya  sumu wala athari kwa Jamii.

Alimalizia kwa kutaka Watanzania kupenda bidhaa zinazotengenezwa  ndani ya nchi na kuwatia moyo wafanyabiashara ili kutengeneza ajira hapa nchini.

Habari Zifananazo

Back to top button