Mil 3/- zakabidhiwa vituo vya yatima Mtwara

MTWARA: JUKWAA la vyama vya Ushirika Mkoa wa Mtwara limekabidhi msaada wa Sh milioni 3 kwa ajili ya kusaidia vituo mbalimbali vya watoto yatima mkoani humo.
Akizungumza wakati wa ghafla fupi ya kukabidhi msaada huo, Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika kinachohudumia wakulima wa wilaya za Tandahimba na Newala (TANECU) Karim Chipola amesema lengo la kutoa msaada huo ni kuwapa faraja watoto ambao wana mahitaji maalumu ili na wao waweze kutimiza malengo yao bila kuwa na kikwazo chochote.
Amesema kutokana na changamoto zinazowakabili kwenye vituo hivyo ushirika huo utaweke utaratibu maalumu wa kuhakikisha kila mwaka unatekeleza zoezi hilo na kuwaahidi kuwa kila wanapopata changamoto wao wako tayari kuwashika mkono.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu na Huduma za Jamii katika Jukwaa hilo, Paul Anania amesema msaada huo uliyotolewa ni mahitaji muhimu ambayo viongozi wa vituo hivyo walibainisha ikiwemo vifaa vya shule na vingine..
“Kwa kiasi kikubwa ni vifaa vya shule katika kituo cha Mikindani Yatima Foundation kilichopo Mikindani na miongoni mwa vidaa vilivyotolewa ikiwemo jora za vitambaa kwa ajili ya kushona sale za shule, madaftari, rula na katoni za juisi vyenye ghalama ya shilingi milioni 1.5″amesema Paul
Aidha kituo kingine ni cha Upendo Liabilitation Center kilichokabidhiwa msaada wa Pampasi, sabuni, mafuta, unga, mchele, vinywaji na vingine vyenye thamani ya Sh milioni 1.5 na kuahidi kuwa wataendelea kuboresha ili jukwaa la mwakani (2026) waweze kuwafikia watu wengi.
Akitoa shukrani zake juu ya msaada huo, Meneja wa Kituo cha Upendo Liabilitation Center kilichojikita zaidi na kulea watoto wenye mahitaji maalumu wakiwemo wenye usonji, ulemavu wa viongo na wengine, Faustin Keha amesema msaada huo utawasaidia kwa kiasi kikubwa katika mahitaji ya watato hao.
Kaimu Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Mtwara, Robert Isuza amewapongeza wana Ushirika mkoani humo kwa kujitoa kwa wanajamii kwa kuanzia zoezi hilo ngazi ya halmashauri na kutamatisha kutoa kwa mkoa huku akiwasihi kuendelea kushikamana na kuendelea kujali na kuthamini jamii zinazo wazunguka.