Mila potofu zatajwa kukwamisha chanjo kwa watoto

MENEJA wa Mpango wa Chanjo Taifa, Dk Florian Tinuga amesema mila potofu za jamii ya kuhamahama makazi yao ni moja ya changamoto ya watoto kutopatiwa chanjo hali inayopelekea athari ya kiafya kwa watoto.

Akizungumza na waandishi wa habari katika semina elekezi ya Mpango wa Taifa wa Chanjo kutoka mikoa ya Kanda ya Kaskazini, Dk Tinuga amesema njia ya kuondoa dhana hiyo ni elimu kwa wazazi na walezi.

Amesema mila potofu huwa hazitokei sana kwa chanjo ya watoto chini ya umri wa miaka mitano na badala yake changamoto inatokea kwa wenye umri zaidi ya hapo.

Amesema chanjo inayoingizwa nchini ikiwa na tatizo kutokana na kuwa na jopo la wanasayansi ambao imeteuliwa na Waziri wa Afya kwa ajili ya kuthibitisha matumizi yake.

“Sisi Mpango wa Taifa wa Chanjo tunasimamia chanjo katika makundi manne ikiwa kundi la kwanza ni  chanjo za watoto chini ya miaka mitano, HPV kwa upande wa wanawake na wasichana wenye umri wa miaka 14 na bado mwitiko wake ni mdogo hususani kwenye dozi ya pili,”amesema Dk Tinuga.

Aidha amesema kundi la tatu ni chanjo dhidi ya wajawazito ikiwa hiyo haina changamoto yoyote bali ni pale mama mjamzito anapochelewa kwenda kliniki ndio madhara yake yanapojitokeza katika kumwathiri yeye au mtoto na la mwisho ni chanjo ya Uviko 19 iliyoanzishwa mwaka 2021.

Amesema sasa hivi chanjo hizo zinapatikana katika vituo vyote vya afya nchini kwa asilimia 100 ila changamoto ipo katika matumizi yake watu kufika ili kupatiwa huduma hiyo.

Mganga Mkuu wa Mkoa Arusha Dk Sylvia  Mamkwe amesema hakuna haja ya wanawake na watoto wa kike kuogopa kupima saratani ya shingo ya kizazi sababu ni moja ya saratasni inayotibika na kuepukana na kifo.

Vile vile ni muhimu kwa kila mmoja kuhimiza watoto wa kike wenye umri wa miaka 14 kupata chanjo ya kuzuia saratani hiyo ili kulinda kizazi kijacho.

“Katika saratani ambazo zinatibika ni hii ya saratani ya shingo ya kizazi inatibika na serikali imewekeza nguvu kubwa ili kuokoa watu. Tusiogope  kipimo hakiumi, lakini watoto wa kike wapate hii chanjo ili kulinda kizazi kijacho,”amesema.

Pia Dk Mamkwe ameshukuru serikali kwa kuboresha sekta ya afya na kwa Mkoa wa Arusha, wamepokea zaidi ya Sh bilioni 20 kwa ajili ya maboresho ya sekta hiyo na kupokea vipimo vikubwa, hivyo muhimu kwa wnaanchi kujitokeza kupima afya zao ili kujilinda zaidi

Ofisa Mpango wa Taifa wa Chanjo Wizara ya Afya, Lotalis Gadau  amesema mafunzo hayo yanatolewa mikoa yote kwa nyakati tofauti ili kujenga uelewa wa pamoja kuhusu masuala ya chanjo mbalimbali

Amesema nyumba ni mwanamke hivyo muhimu kuwalinda watoto wa kike ambao ni wamama watarajiwa wa baadaye.

“Hawa ni muhimu kuchanjwa ili kuwalinda,lakini kwa wale wanaopatikana mapema wakiwa na saratani  kuna dawa wanapewa na kupona,wakichelewa ni madhara makubwa yanayosababisha baadhi yao kupoteza maisha,”amesema.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
neknoyirze
neknoyirze
3 months ago

I get paid more than $90 to $100 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this I have earned easily $21k from this without having online working skills . Simply give it a shot on the accompanying site…

Here is I started.…………>>
http://www.join.hiring9.com

Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x