KLABU ya Pamba Jiji imemteua Fred Felix ‘Minziro’ kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo.
Taarifa ya Pamba Jiji iliyotolewa leo na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu Ezekiel Ntibikeha imesema Minziro atashirikiana na Kocha Msaidizi, Mathias Wandiba.
SOMA: Kopunovic ndio basi tena Pamba Jiji
“Uongozi wa Klabu ya Pamba Jiiji Fc, unautaarifu umma kuwa umeingia makubaliano na kocha Fred Felix ‘Minziro’ kuwa Kocha Mkuu akichukua mikoba ya Goran Kopunovic,” imesema taarifa hiyo.
Taarifa hiyo imesema kwa uteuzi huo wanamwanza wana matumaini kuiona Pamba Jiji ikifanya vizuri Ligi Kuu Tanzania Bara.
Pamba Jiji inashika nafasi ya 16 mwisho wa msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 4 baada ya michezo 7, haijashinda mechi yoyote, imetoka sare 4 na kupoteza 3.