DAR ES SALAAM – WACHEZAJI Luis Miquissone na Shabani Chilunda wameingia kwenye orodha ya nyota waliopewa mkono wa kwaheri na Klabu ya Simba.
Wachezaji wengine ambao Simba ilitangaza kuachana nao ni aliyekuwa nahodha wao John Bocco na Saido Ntibazonkiza.
Mtandao wa kijamii wa klabu hiyo jana ulitangaza Miquissone na Chilunda waliosajiliwa wakati wa usajili wa msimu wa 2023/24, hawatakuwa sehemu ya kikosi cha Wekundu hao wa Msimbazi msimu ujao.
Miquissone alisajiliwa na Simba kama mchezaji huru baada ya kuvunja mkataba wake na Al Ahly ya Misri wakati Chilunda akisajiliwa na Simba akitokea Azam.
SOMA: Majaliwa aikubali Smartwasomi
Winga huyo wa kimataifa wa Msumbiji kwa mara ya kwanza alisajiliwa na Simba msimu wa mwaka 2020/21 kutoka Ud Songo aliyokuwa kwa mkopo akitokea Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.
View this post on Instagram