QATAR: WAPATANISHI wa Marekani na mataifa ya Kiarabu wamepiga hatua kubwa kuelekea makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas, pamoja na kuachiliwa kwa mateka wanaoshikiliwa na Hamas katika Ukanda wa Gaza.
Maafisa wanne wamekiri kwamba kumepigwa hatua muhimu na kueleza kuwa siku zijazo zitakuwa na umuhimu mkubwa katika kufikia makubaliano ya kusitisha vita vya zaidi ya miezi 15 ambavyo vimevuruga eneo la Mashariki ya Kati.
Maafisa hao wamezungumza kwa masharti ya kutotajwa majina kwa sababu hawajaruhusiwa kujadili mazungumzo hayo yanayoendelea mjini Doha, Qatar.
SOMA: Biden Netanyahu wajadili kusitisha mapigano Gaza
Afisa mmoja wa Marekani amesema pande zote mbili ziko karibu kufikia makubaliano, lakini ametahadharisha kuwa hali inaweza kubadilika wakati wowote.