ZANZIBAR: RAIS wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi amekutana na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Tanzania, Shigeki Komatsubara aliyefika leo kujitambulisha Ikulu Zanzibar.
Katika mazungumzo yao wamegusia uhusiano na ushirikiano uliopo kati ya Zanzibar na UNDP pamoja na kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo, uchumi wa buluu, utalii, Mahakama, kujenga uwezo kwa Taasisi mbalimbali za Serikali ikiwemo Taasisi ya Afisi ya Rais Ufuatiliaji na Usimamizi wa Utendaji Serikalini (PDB) na nyinginezo.