Mkakati kilimo hai kutunza asili waja

DAR ES SALAAM:Taasisi ya Kilimo hai nchini (TOAM) imepanga kuzindua mkakati wa kilimo hai wenye kuhimiza umuhimu wa kutunza asili Kwa ajili ya uendelevu wa afya na mazingira kwa ujumla.

Aidha imeomba serikali kutenga sehemu ya fedha kwaajili ya kilimo hai hata katika miradi mbalimbali ya kilimo inayoendelea nchini ukiwemo ule wa kuwezesha vijana katika kilimo (BBT).

Mtendaji Mkuu wa TOAM, Bakari Mongo amesema hayo leo Dar es Salaam wakati akizungumzia mkutano wa tatu wa kitaifa wa kilimo haiĀ  (NEOAC) unaotarajiwa kufanyika Novemba 8 Hadi 9,2023 mkoani Dodoma.

Mongo amesema katika mkakati huo umeshirikisha wadau mbalimbali ikiwemo serikali, na utazinduliwa katika mkutano huo ili kuboresha mnyororo mzima wa kilimo kuanzia uzalishaji wa mazao mbalimbali.

“Mkakati huo unawalenga wazalishaji kuwa na kilimo endelevu lakini pia ukiangalia suala la afya ya udongo na hata mbegu kwa ujumla,” amesema Mongo.

Kuhusu ushiriki wa kilimo hai kwenye miradi ya kilimo nchini, Mwenyekiti wa Kilimo hai Tanzania Dk Mwatuma Juma ameshauri serikali kutenga kiwango cha fedha ili kilimo hai kuwezesha kutekelezwa nchini.

Ametolea mfano wa mradi wa BBT, kuwa iwapo serikali ina fedha za utekelezaj ione umuhimu wa kuwezesha kilimo hicho lakini pia upande mwingine wao waelimishe kuhusu kilimo hai.

“Kama serikali imekiri kuwa inazo fedha dola za Marekani milioni 160, Kwa ajili ya BBT ione umuhimu wa kutenga hata dola 1000 kwa ajili ya wadau kutekeleza mradi wa kilimo hai,”amesema Mwatima.

Amesema kilimo hai sio suala la wakulima pekee bali pia ni la walaji Ili waweze kusema wanachokitaka kwamba watumie mazao yenye msingi wa afya zao.

 

 

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button