Mkonge wamvuta mwana wa mfalme nchini

Mwana wa mfalme Mwana wa mfalme

BODI ya Mkonge Tanzania (TSB) imesema iko tayari kushirikiana na Falme ya Babina Noko Ba Mampuru iliyopo katika Jimbo la Limpopo nchini Afrika Kusini kuendeleza mkonge.

Ushirikiano huo utahusu mambo mbalimbali ikiwamo kutoa wataalamu wake na kubadilishana uzoefu.

Kaimu Mkurugenzi wa TSB, Saddy Kambona alisema hayo jana wakati akizungumza na Mwana wa Mfalme wa Falme ya Babina Noko Ba Mampuru, Spumendo Mokgabudi aliyemtembelea ofisini kwake jijini Tanga.

Advertisement

Mokgabudi yuko nchini kwa ziara binafsi kwa ajili ya kufanya utafiti na kujifunza mambo mbalimbali kuhusu zao na kilimo cha mkonge akiwa na mpango wa kuanzisha kilimo hicho kwenye falme yake.

Akiwa Tanga alikutana na Menejimenti ya Bodi ya Mkonge na uongozi wa Kampuni ya D.D. Ruhinda.

Katika mazungumzo yao, Mokgabudi alimwomba Kambona kumsaidia mambo matatu ikiwamo kuiomba Bodi ya Mkonge imsaidie upatikanaji mbegu za mkonge kwa ajili ya falme yake.

Mokgabudi akiwa na Menejimenti ya Bodi ya Mkonge na uongozi wa Kampuni ya D.D. Ruhinda.

 

 

 

 

“Tumepata ugeni wa Mwana wa Mfalme kutoka Afrika Kusini, tumezungumza mengi lakini kikubwa ni kuhusu suala zima la zao la mkonge na miongoni mwa mambo aliyoomba mbali na upatikanaji wa mbegu ni kubadilishana wataalamu ambao watakuja nchini na wa hapa nchini kwenda kule ili kujifunza mambo mbalimbali,” alisema.

“Tuko tayari kushirikiana na kampuni hiyo ya Babina Noko Mampuru kwa kutoa wataalamu wa zao la mkonge kwa ajili ya kwenda kutoa mafunzo kwa wataalamu wengine wa falme hiyo nchini Afrika Kusini,” alisema.

 

Aliongeza: “Lakini pia tumekubaliana kubadilishana uzoefu kwa kubadilishana wataalamu wetu ambao watakuwa wanakuja huku na wa kwetu wanakwenda kule.”

Kwa upande wake, Mokgabudi alisema atarudi wakati mwingine ili kujifunza zaidi kwa kuzunguka maeneo mengi  kwani hiyo ni ziara yake binafsi nchini.

Alisema katika mikakati ya kuanzisha kilimo cha mkonge nchini Afrika Kusini tayari wana hekta milioni tatu zilizotengwa kwa ajili hiyo.

Mkurugenzi wa Kampuni ya D.D Ruhinda Ltd, Deo Ruhinda alisema ushirikiano huo utaleta tija.

 

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *