Mkongo wa 2 Africa Submarine kupaisha uwezo wa tehama

TANZANIA itakuwa kitovu cha maunganisho ya mawasiliano Afrika Mashariki na Kati kutokana na uwepo wa mkongo wa mawasiliano wa 2 Afrika utakapokamilika Februari mwakani.

Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk Jim Yonazi alipofanya ukaguzi wa mkongo wa kituo cha 2 Afrika juzi na kueleza kuwa hilo linafanyika kutokana na juhudi za serikali kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha maunganisho ya mawasiliano.

Alisema kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho una faida kubwa kwa nchi kwa kupata mtandao wa intaneti yenye kasi zaidi na uhakika wa kuunganishwa duniani.

“Mkongo unaokuja unapitia Kusini mwa Bara la Afrika, kwa hiyo tutapata uhakika wa maunganisho kwenda duniani na kusaidia biashara ya kuuza uwezo nchini mwetu na nchi jirani na kuwasaidia wananchi wetu na nchi jirani kuweza kushiriki katika uchumi wa kidijiti ambao ndio uchumi sasa dunia inashiriki,” alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Masuala ya Udhibiti na Mawasiliano, Beatrice Singano alisema wanatengeneza eneo la kusambaza mawasiliano yanayopitia baharini ili kuiwezesha Tanzania kufikiwa na kufikia maeneo mengine kimawasiliano.

Singano ameeleza kuwa mkongo huo unatokea Djibouti na unahimili kwa kiwango kikubwa uwezo wa kutoa mawasiliano tofauti na hapo awali na kuiwezesha Tanzania kukua kimawasiliano na huduma hiyo itanufaisha pia nchi jirani.

Mkongo huo mpya wa kisasa utakaotoa mawasiliano ya kasi kiasi cha terabytes 180 TB ni mmoja kati ya mkongo mkubwa duniani utakaotokea Bara la Ulaya na kukatiza Mashariki ya Kati kwa kupitia nchi mbalimbali za Afrika hadi nchini.

Mkongo wa 2 Africa Submarine unatarajiwa kukamilika mwanzoni mwa mwaka 2023 kwa kufika katika zaidi ya maeneo 35 katika nchi 26 duniani.

 

 

 

 

 

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x